Tambua dalili, kinga na tiba ya mdudu asali kwenye tikiti maji.
Mdudu asali ni wadudu wadogo wanaonyonya maji kwenye majani ya tikiti maji. Wadudu hawa husababisha kudhoofika kwa mmea na kuenea kwa magonjwa ya virusi.
jani hili lina utando kama vile limepakwa asali au mafuta
Ukigeuza upande wa chini wa jani la tikiti utaona wadudu wenye rangi ya kijani . kitaalamu huitwa (aphidi)
jani lililo jikunja baada ya kushambuliwa na wadudu
Ili kupunguza madhara ya mdudu asali kwenye tikiti, tumia njia zifuatazo:
Ni kiua dudu kinachopenyeza ndani ya mmea kuua wadudu kama sumu ya tumbo au mguso
matumizi yake yameandikwa katika kipepelushi cha dawa usika pia unaweza pokea maelezo kutoka kwa bwana shamba
Vitunguu vina harufu kali inayotolewa na misombo ya sulfur kama allicin. Harufu hii inawachanganya na kuwazuia wadudu kama aphids, whiteflies, na thrips, wasikaribie mimea ya tikiti maji.
Panda mistari ya vitunguu kati ya mistari ya tikiti maji
Hakikisha vitunguu vinapandwa kabla ya msimu wa aphids kuanza ili viwe tayari kutoa kingaUnaweza pia kusaga vitunguu na kupulizia maji yake kwenye majani kama dawa ya asili
fahamu njia za kupambana na wadudu pia na wanyama washambuliao matikiti
SomaJinsi ya upandaji wa tikiti
Somajinsi ya kuzuia matikiti kuoza shambani
SomaFahamu njia za kujua kua tikiti limeiva (komaa) tayali kwa biashala au kuliwa
SomaNamna sahihi ya uchimbaji wa mfereji ya maji katika shamba la tikiti
SomaJe ni mda gan sahihi wa kukata maji(kusimama umwagiliaji) ili kuhakikisha tikiti lina sukali ya kutosha
SomaFahamu ardhi nzuli kwa ulimaji wa tikiti
SomaKwann tikiti zako haziwi na maumbo makubwa? .Fahamu njia zitakazo kukusaidia kupata tikiti zenye maumbo makubwa
Soma© Kilimo Bora - Tovuti yako ya maarifa ya kilimo.