Tambua dalili, kinga na tiba ya mdudu asali kwenye tikiti maji.
Mdudu asali ni wadudu wadogo wanaonyonya maji kwenye majani ya tikiti maji. Wadudu hawa husababisha kudhoofika kwa mmea na kuenea kwa magonjwa ya virusi.
Ili kupunguza madhara ya mdudu asali kwenye tikiti, tumia njia zifuatazo:
Ni kiua dudu kinachopenyeza ndani ya mmea kuua wadudu kama sumu ya tumbo au mguso
matumizi yake yameandikwa katika kipepelushi cha dawa usika pia unaweza pokea maelezo kutoka kwa bwana shamba
Vitunguu vina harufu kali inayotolewa na misombo ya sulfur kama allicin. Harufu hii inawachanganya na kuwazuia wadudu kama aphids, whiteflies, na thrips, wasikaribie mimea ya tikiti maji.
Panda mistari ya vitunguu kati ya mistari ya tikiti maji
Hakikisha vitunguu vinapandwa kabla ya msimu wa aphids kuanza ili viwe tayari kutoa kingaUnaweza pia kusaga vitunguu na kupulizia maji yake kwenye majani kama dawa ya asili